Monday, January 23, 2012

CHANETA VS CHANEZA KIKAONI

CHANETA VS CHANEZA KIKAONI



Chama cha Netiboli Tanzania Bara (CHANETA) na wenzao wa Zanzibar (CHANEZA) wanatarajia kukaa pamoja Jan 28, mwaka huu.
CHANETA na CHANEZA watakaa pamoja kujadili maendeleo ya mchezo huu nchini. 

POLISI DOM YAANZA POA

POLISI DODOMA YAANZA VIZURI
Timu ya Polisi Dodoma imeanza vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu kwa kuibamiza JKT bao 1-0 katika uwanja wa Azam wa Chamazi.
Kwa ushindi huo Polisi imeshika nafasi ya 12 katika msimamo JKT ikiwa nafasi ya 7 na ina pointi 17.

NCHUNGA AMJIA JUU PAPIC

NCHUNGA AMJIA JUU PAPIC
Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amemjia juu kocha wa Yanga Mserbia Kostadic Papic kwa tabia yake ya kuzungumza na waandishi mara kwa mara.
Nchunga amesema tabia ya Papic kutoa taarifa za timu bila ruhusa ni kuwavuruga wanachama.

Saturday, January 21, 2012

TWIGA STARS KURUDIANA NA NAMIBIA (AWC)

TWIGA STARS KURUDIANA NA NAMIBIA (AWC)
Mechi ya marudiano katia ya Twiga Stars na Namibia itachezwa itachezwa Januari 29 jijini Dar es Salaam.
Twiga Stars itashuka dimbani ikiwa na rekodi ya 2-0 katika mchezo wa awali.
Mechi hii ya marudiano itarushwa moja kwa moja na ITV. 

NJOROGE AVUNA PESA YANGA

NJOROGE AVUNA PESA YANGA
Timu ya Yanga inatakiwa kumlipa jumla ya shilingi milioni 17,159,800 za Tanzania beki wa kimataifa wa Kenya na Sofapaka John Njoroge.
Yanga imeamriwa kulipa pesa hizo na FIFA ndani ya siku 30.

LIGI KUU RAUNDI YA PILI KUANZA LEO

LIGI KUU RAUNDI YA PILI KUANZA LEO

Ligi Kuu ya VodaCom Tanzania Bara, itaanza leo baada ya kupumzika kwa kipindi fulani.
Mechi zitapigwa leo katika viwanja tofauti ambapo mabingwa watetezi Yanga itavaana na Moro Utd katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Mtibwa Sugar itapambana na JKT Oljoro huku Ruvu Shooting ikipambana na Toto Afrika kwenye uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.  

Tuesday, January 10, 2012

GOLI BORA LILILOFUNGWA KIPA

GOLI BORA LA KIPA LILILOFUNGUA MWAKA 2012
Hili naliita goli bora lililofungua mwaka huu mpya wa 2012, lililofungwa na golikipa Tim Howard wa Everton katika mechi waliyokutana na Bolton Wanderers ambayo walifungwa bao 2-1.