PAUL KAGAME, MOISE KATUMBI NA WAAFRIKA 
WATANO WAPENDA SOKA
Makala hii inaangalia Waafrika watano wanasiasa na wafanyabiashar maarufu ambao mapenzi yao katika soka nyameleta mageuzi katika mchezo huu barani Afrika.
 Klabu nyingi barani Afrika zinaendelea (surviving) kwa sababu zinasapotiwa kwa karibu na mwansiasa au mfanyabishara mkubwa. Baadhi wanafadhili vilabu wavipendavyo hadharani na baadhi wafadhili kutokea nyuma ya pazia.
Wanasiasa hujiingiza michezoni kuongeza kuungwa mkono kwao na wananchi na wafanyabiashara wenye ndoto za kisiasa hujiingiza katika soka ili kupima umaarufu wao.
Ifuatayo ni list na maelezo ya baadhi ya watu mashuhuri Afrika:-
1.   PAUL KAGAME (RWANDA)
Rais wa Rwanda Paul Kagame (54) mwendawazimu wa soka (Footbal Aficianado) na kama ilivyo kwa Waafrika wengi nae ana mapenzi na timu za Ulaya Man. Rais Kagame binafsi amedhamini mashindano ya soka katika nchi yake na Afrika Mashariki ili kukata kiu yake ya mapenzi ya soka. Tokea mwaka 2002, mashindano ya vilabu ya CECAFA timu za Afrika Mashariki na Kati yamedumu/ yamefanyika kutokana na ufadhili wake, mpaka kufikia kuitwa kwa jina lake yaani Kombe la Vilabu la Kagame.
2.   ORJI OZUL KALU (NIGERIA)
Gavana wa Zamani wa jimbo la Abia anse chukuliwa kama muhimili wa mafanikio ya klabu ya Enyimba wakati ilipochukua ubingwa wa Afrika mara mbili mfululizo (2003 na 2004) hii ikiwa ni mbali na mataji lukuki waliyoshinda nchini Nigeria. Alifika kutaka kuiingiza Enyimba katika soko la hisa la Nigeria (Nigeria Stock Exchange).
3.   MOISE KATUMBI (DR CONGO)
Meya wa mji wa Katanga, Moise katumbi amelitumia soka kama chombo cha kuwaunganisha vijana katika mji wenye kujulikana kwa rabsha (restive situations). Katumbi ndiyo mfadhili wa moja ya klabu zenye mafanikio ya kipekee Afrika, TP Mazembe. Ameibadilisha Mazembe kutoka timu ya kawaida mpaka kuwa timu tishio barani Afrika. Walichukua kombe la klabu bingwa Afrika miaka ya 2009 na 2010 na kuwa klabu ya kwanza kushika nafsi ya pili katika mashindano ya Dunia ya Vilabu mwaka 2010. Kutokana na pesa zake wanasoka wa Kongo wamejulikana duniani kote.
4.   PATRICE MOTSEPE (SOUTH AFRICA) 
5.   DR. KWAME NKRUMAH (GHANA)
Nkrumah ndiye alikuwa rais wa kwanza wa Ghana. Wanahistoria wanasema hakuna hadithi ya soka la Afrika bila ya kumtaja Nkrumah. Alikuwa ni muumini mkubwa wa soka na michezo kwa ujumla, na aliitumia kuendeshea hoja yake ya Muungano wa Afrika. Ni mmoja wa waanzilishi wa Shirikisho la Vyama vya soka Afrika (CAF) na inasemekana alichangia 250 Guineas katika kombe la Osagyefo. Kuanzisha kombe la vilabu Afrika mwaka 1964 amablo sasa linajulikana kama Kombe la Mabingwa CAF.