RATIBA YA EURO 2012 POLAND & UKRAINE KESHO 02/12/2011
POLISI WAKABIDHI FAILI LA JOHN TERRY KWA MWENDESHA MASHITAKA
John Terry
BREAKING NEWS: LUCAS LEIVA NJE MIEZI 7
Lucas Leiva
LIVERPOOL YAMUALIKA MCHEZAJI WA NY RED BULLS KWA MAJARIBIO
Juan Sebastian Agudelo
YA SIMBA NA BASENA VICHEKESHO!!!
SNAKE BOY KUZICHAPA NA MTAMBO WA GONGO
RAMADHAN CHOMBO "Redondo" abaki AZAM FC
Macho na masikio ya mamilioni ya wapenzi wa soka duniani kesho 02/12/2011 yataelekezwa huko Kiyev, Ukraine kushuhudia upangaji wa ratiba ya EURO 2012.
Wengi wana hamu ya kujua ni nani atakuwa na bahati mbaya ya kupangwa na mabingwa watetezi Spain, au timu inayopewa nafasi kubwa kufanya vizuri ya Ujerumani au timu iliyosheheni vipaji ya Uholanzi. Tuombe uzima tushuhudie ratiba na fainali zenyewe hapo June mwakani Inshaallah.
POLISI WAKABIDHI FAILI LA JOHN TERRY KWA MWENDESHA MASHITAKA
John Terry
Polisi wa Uingereza kitengo cha uchunguzi (Scotland Yard), wamekamilisha uchunguzi wa kesi ya kutoa maneno ya kibaguzi inayomkabili beki wa Chelsea John Terry dhidi ya mchezaji wa QPR Anton Ferdinand.
Hata hivyo mwendesha mashitaka ameeleza kuwa ataangalia kama kesi hiyo ina ushahidi wa kutosha kuipeleka mahakamani na kama hakuna ushahidi ataitupa. Tusubiri tuone.
BREAKING NEWS: LUCAS LEIVA NJE MIEZI 7
Lucas Leiva
Liverpool imetangaza kuwa kiungo wake tegemeo Lucas Leiva ameumia vibaya goti la kushoto na atakuwa nje kwa muda wote wa ligi uliobaki.
Lucas anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti hilo hivi karibuni. Kuumia kwa kiungo mkabaji huyu ni pengo kubwa kwa Liverpool ambayo ametokea kuwa mchezaji muhimu sana. Tunamtakia Lucas kupona kwa haraka.
LIVERPOOL YAMUALIKA MCHEZAJI WA NY RED BULLS KWA MAJARIBIO
Juan Sebastian Agudelo
Liverpool imemualika mshambuliaji wa Kimataifa wa Marekani anayechezea New York Red Bulls Juan Sebastian Agudelo kwa majaribio.
Agudelo 19, ana asili ya Colombia ameicheza timu ya taifa ya Marekani mechi 15 na kuifungia magoli 2.
Anacheza timu moja na Thierry Henry.
MARK HUGHES ATAJWA KUMBADILI STEVE BRUCEKocha alietimuliwa Steve Bruce (L) akiwa
na kocha mtarajiwa Mark Hughes
na kocha mtarajiwa Mark Hughes
Kocha asiyekuwa na kibarua Bw. Mark Hughes anatajwa kuwa ndio chaguo la kwanza la uongozi wa Sunderland kuchukua mikoba Bw. Steve Bruce alietimuliwa kazi jana.
Hughes ameonana na uongozi wa Sunderland kwa ajili ya usaili na anapewa nafasi kubwa na wachambuzi kupata nafasi hiyo. Hata hivyo anapata upinzani mkubwa kutoka kwa kocha mwingine mahiri Martin O'Neill.
Sunderland wapo katika mapambano ya kujinasua kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 16 katika msimamo wa EPL. Tusubiri Breaking News!
YA SIMBA NA BASENA VICHEKESHO!!!
Ofisa Habari wa timu ya Simba SC Bw. Ezekiel Kamwaga ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa klabu yake imemtimua kazi kocha wao Moses Basena kutokana na kushindwa kuwasilisha vyeti vyake vya elimu. Nafasi yake imechukuliwa na Milovan Cirkovic wa Serbia aliyesaini mkataba wa miezi sita.
Uongozi wa Simba ulimpa mkataba wa miezi sita Basena kabla ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili unaotarajiwa kuisha September 2013. Kwa kuuvunja mkataba wake Simba itapaswa kumlipa Basena zaidi ya Sh.95milioni kama fidia pesa ambayo ni nyingi sana.
Swali la kuuliza uongozi wa Simba, waliwezaje kumwajiri mtu ambaye hawajaona vyeti vyake vya elimu na kuvihakiki?? Na kama kweli Basena hana vyeti aliwezaje kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Uganda??? Watanzania tuna haki ya kuujua ukweli.
SNAKE BOY KUZICHAPA NA MTAMBO WA GONGO
Rashid Matumla
Bondia mkongwe Rashid Matumla "Snake Boy" aliyetikisa anga za masumbwi miaka ya tisini anatarajiwa kuzichapa na bondia machachari nchini Maneno Oswald "Mtambo wa Gongo" tarehe 25/12/2011.Mabondia hao wana rekodi ya kukutana mara 3 (Matumla akishinda 2 na Maneno 1).
Hata hivyo mashabiki wengi waliotoa maoni yao kwa Spoti Kizaazaa wameonyesha wasiwasi wao kutokana na umri mkubwa alio nao Snake Boy na kujiuliza kama kweli ataweza kuendana na kasi kubwa ya makonde ya Mtambo wa Gongo? Tusubiri na kuona inshaallah
Mchezaji wa timu ya soka inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara maarufu kama VodaCom Premier League (VPL) Ramadhan Chombo "Redondo" amekataa kujiunga kwa mkopo katika timu ambayo viongozi wa Azam FC walitaka kumpeleka, lakini taarifa za uchunguzi zinaonyesha kutokuwa na maelewano baina mchezaji huyo na uongozi.
Taarifa zinasema viongozi wa Azam FC walitaka kumuuza japo kwa mkopo, lakini baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu aamua kuendelea na timu yake ya Azam FC (Wanalambalamba) au watoto wa Chamanzi.
Hii blog nimeikubali jamaa...
ReplyDeletePiga Kazi tupo Pamoja @Mdau Cairo
ReplyDelete