Friday, December 2, 2011

Dondoo

NGORONGORO HEROES 3-3 ZAMBIA COSAFA CUP
Bendera ya Tanzania
  Timu ya taifa ya Tanzania ya (U-20) imetoka sare ya magoli 3-3 na wenzao wa Zambia katika mashindano ya COSAFA U-20 yanayoendelea nchini Botswana. Vijana wa Zambia walikuwa na kibarua kigumu cha kurudisha magoli yaliyokuwa wanafungwa.
Wafungaji wa magoli kwa upande wa Tanzania ni Simon Happygod (2) na Hassan Kessy (1).

MAKUNDI EURO 2012 HADHARANI!!!
  Haya haya, hayawi hayawi sasa yamekuwa! Ile kazi ya kupanga makundi ya mashindano ya Euro 2012 imekamilika na sasa mambo yako hadharani kweupeeee! Makundi yamepangwa hivi:

KUNDI A: POLAND, GREECE, RUSSIA, CZECH REPUBLIC

KUNDI B: NETHERLANDS, DENMARK, GERMANY, PORTUGAL

KUNDI C: SPAIN, ITALY, REP. OF IRELAND, CROATIA

KUNDI D: UKRAINE, SWEDEN, FRANCE, ENGLAND 

Wadau mnasemaje kuhusu huu mtanange??? Mimi naona hatumwi mtoto dukani! Mungu atupe uhai kushuhudia utamu huu inshaallah.


MUHAMMED ALI AKIMBIZWA HOSPITALI
Muhammed Ali alipohudhuria mazishi ya Joe Frazier mwezi uliopita
  Gwiji wa masumbwi wa zamani Mohammed Ali alikimbizwa katika hospitali ya Scottsdale Healthcare Osborn Medical Center juzi kutokana na kuanguka na kupoteza fahamu akiwa nyumbani kwake.
  Hali yake imeleta wasiwasi mkubwa kwa wanafamilia na wapenzi wa bondia huyo wa zamani.
  Mara ya mwisho kuonekana hadharani kwa bondia huyo ilikuwa ni katika mazishi ya bondia Joe Frazier 14.Novemba.2011 huko Philadelphia.
  Kwa sasa Muhammed Ali anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitali. Tunamuombea Mungu hali yake ya kiafya iimarike.


NGORONGORO HEROES UWANJANI LEO
Bendera ya Tanzania
  Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania chini ya miaka 20 (U-20) inashuka dimbani leo majira ya saa 12:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kupambana na Zambia katika michuano ya Shirikisho la soka la Nchi za Kusini mwa Africa (COSAFA). 
  Ngorongoro Heroes inashiriki kama timu mwalika katika mashindano hayo yanayofanyika Gaborone, Botswana.


TANZANIA YAWA YA PILI GOFU
  Mcheza gofu wa Tanzania Madina Idd ameshika nafasi ya pili katika mashindano ya liyofanyika nchini Uganda.
  Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mchezaji kutoka Uganda. Hongera Madina, ongeza juhudi zaidi.

RIADHA MAMBO SI SHWARI
  Katika hali isiyo ya kawaida chama cha riadha cha mkoa wa Dar es Salaam (DAAA) kimesogeza mbele uchaguzi wake mpaka hapo itakapotangazwa tena.
  Wakati huo huo Chama cha Riadha Tanzania (RT) nacho kimesogeza mbele uchaguzi wake. Katibu mkuu wa RT Bw. Suleiman Nyambui alisema uchaguzi utafanyika Januari 2012 na si Desemba 2011 tena kama ilivyopangwa mwanzo.

No comments:

Post a Comment

Post a Comment