SOKA: NUSU FAINALI CHALENJI HAPATOSHI!
SOKA: WANAWAKE WAPATA MWENYEKITI
SUDAN vs RWANDA
UGANDA vs TANZANIA
Leo ndio leo... Timu ya taifa ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" leo 10:00 alasiri inashuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Chalenji kwenye uwanja wa Taifa.
Kili Stars ambao ni mabingwa watetezi wameingia hatua hii baada ya kuifunga timu ya taifa ya Malawi "The Flames" kwa bao 1-0. Nayo timu ya taifa ya Uganda wao waliitoa timu ngumu ya taifa ya Zimbabwe kwa bao 1-0.
Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa saa 8:00 mchana utakaozikutanisha timu ya taifa ya Rwanda "Amavubi" dhidi ya timu ya taifa ya Sudan "Desert Hawks".
Washindi wa mechi za leo wanatarajiwa kuumana katika fainali siku ya Jumamosi 10.12.2011 katika uwanja wa Taifa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kili Stars.
Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) mkoa wa Pwani kimepata Mwenyekiti mpya na wajumbe katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi hizo, baada ya nafasi hizo kuwa wazi kwa kipindi kirefu.
Katika uchaguzi huo ulio uliofanyika katika ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), ambapo Isege Mabula alichaguliwa kuwa Mwenyekiti. Nafasi ya Katibu Msaidizi ilinyakuliwa na Saumu aliyekuwa mgombea pekee. Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu ilienda kwa Lydia Masena aliyemshinda Magdalena Mwinuka.
Wajumbe 9 kutoka wilaya za Mafia, Rufiji na Mkuranga hawakuhudhuria uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment