SUNDERLAND YAMWAJIRI KOCHA MARTIN O'NEILL
KILIMANJARO STARS KIBARUANI TENA
GOLF: LUGALO OPEN 2011 KUANZA
Martin O'Neill (59) amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu ya soka ya Sunderland inayoshiriki Ligi kuu ya Uingereza.
O'Neill ameziba nafasi iliyoachwa wazi na Steve Bruce aliyetimuliwa katikati ya wiki. Kazi kubwa ya O'Neill ni kujaribu kuitoa Sunderland katika janga la kushuka daraja. Kwa sasa ipo nafasi ya 16.
KILIMANJARO STARS KIBARUANI TENA
Timu ya Taifa ya mpira ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) leo inashuka tena dimbani kuumana na timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kilimanjaro Stars maarufu kama "Kili Stars" inahitaji japo sare ili kupata nafasi ya kufuzu, kabla ya mechi hiyo kutakuwa na mechi kali kati ya Kenya (Harambee Stars) ikiumana na Sudan katika mfululizo wa mashindano haya.
Mashindano ya mchezo wa Golf ya Lugalo Open 2011 yanatarajiwa kuanza leo katika viwanja vya Lugalo huku yakishirikisha zaidi ya wachezaji 100.
Akizungumzia mashindano hayo, Ofisa Mtendaji wa Chama cha Golf Tanzania (TGU), Sophie Nyanjare alisema mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya Coca Cola, TTCL na Tanzania Distilleries Ltd.
Aliendelea kueleza kuwa wachezaji wanaotarajiwa kushiriki ni kutoka katika klabu za Arusha Gymkhana, TPC Moshi, Morogoro, Lugalo na Dar es Salaam Gymkhana.
Rais wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar (BD), Alfred Ngalaliji amesema kuwa mkoa wa DSM utawakilishwa na timu sita ikiwa ni timu 2 kutoka kila wilaya (Ilala, Temeke na Kinondoni).
Mashindano ya kombe la Taifa yanatarajiwa kuanza Desemba 11 yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
RAI KWA WATANZANIA: TUISHANGILIE TIMU YETU TUWAPE MORALI WACHEZAJI
Spoti Kizaazaa inapenda kutoa rai kwa mashabiki na wapenzi wa Taifa Stars kujitokeza kwa wingi leo kuishangilia kwa nguvu timu yetu ya Taifa.Uzalendo ni muhimu sana, na mashabiki ni mchezaji wa 12 katika timu.
Tuache kuzomea, ache kuwakatisha tamaa wachezaji wetu wanapokosea, tuache kushangilia timu za nje na tuwe nyuma ya timu yetu kwa dakika zote 90.
Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment