Thursday, December 15, 2011

Dondoo

PATA HABARI ZA MAKINI ZA MICHEZO YA NDANI, KIMATAIFA, UCHAMBUZI WA KINA...

SOKA: UNAFUNGA GOLI HALAFU RED CARD HIYOOOO!
Mshambuliaji wa Figuirense U20 ajulikanae kama Pottker ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga goli na goli hilo kumsababishia apewe kadi nyekundu.
Kosa lake ni kuwa aligombea mpira uliodundwa na refa na kufunga.
Kwa kawaida refa akidunda mpira wachezaji hufanya "fair play" kwa kutoa pasi kwa timu iliyokuwa inaumiliki kabla ya refa kupiga filimbi
Refa alikubali goli lakini akatoa red kadi kwa mfungaji.
Figuirense U20 ilishinda 4-1 dhidi ya Bahia U20
Jionee mwenyeweee!

SOKA: JERRY SANTO APATA ZALI ALBANIA
JERRY SANTO
Kiungo Mkenya Jerry Santo amejiunga na timu ya KF Tirana ya Albania kwa mkataba wa miaka miwili na nusu. Santo aliyeikacha Simba ya Tanzania na kuelekea Vietnam alipojiunga na timu ya HAGL mapema mwaka huu ambapo aling'ara vilivyo na kufanya klabu mbali mbali kuvutiwa nae.
Kwa sasa Santo anakamilisha nyaraka zake za kusafiria ili kukwepa matatizo yaliyowakuta wachezaji wenzake mshambuliaji Moses Arita wa Thika United na beki James Situma aliyekuwa Sofapaka ambao walichelewa kujiunga na timu zao za Ulaya kutokana na matatizo ya viza.
Santo aliyewahi kuchezea pia Tusker ya Kenya, sasa atajiunga na kundi la Wakenya kibao wanaocheza Ulaya kama kapteni wa Harambee Stars Denis Oliech, McDonald Mariga na Victor Wanyama ambao wote wanacheza klabu za ligi kuu za Ulaya.
Mara ya mwisho Santo kuitwa Harambee Stars ilikuwa kabla ya mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Shelisheli, ambapo alitemwa na kocha Francis Kimanzi.

No comments:

Post a Comment

Post a Comment