Wednesday, December 14, 2011

Dondoo

PATA HABARI ZA MAKINI ZA MICHEZO YA NDANI, KIMATAIFA, UCHAMBUZI WA KINA...

SOKA: KESI YA UBAGUZI WA RANGI INAYOMKABILI 
SUAREZ YAANZA KUUNGURUMA.
Kesi ya kutoa maneno ya kibaguzi inayomkabili mchezaji Luis Suarez wa Liverpool imeanza kusikilizwa na Chama cha Soka cha Uingereza (FA) chini ya usiri wa hali ya juu.
Inaaminika kesi hiyo itachukua siku mbili kusikilizwa huku Suarez na Patrice Evra wa Manchester United wakitarajiwa kutoa ushahidi wao.
Kama FA itamkuta na hatia Suarez, nyota huyu wa Liverpool atarajie adhabu ya  kifungo kirefu cha kuichezea timu yake

SOKA: MECHI DHIDI YA UMASIKINI YAFANA
Mechi ya hisani ya kupambana na umasikini iliyozikutanisha timu ya Marafiki wa Ronaldo na Zidane dhidi ya Wachezaji Nyota wa Humberg Fc (Allstars) imefanyika usiku wa Jumanne 13/12/2011 mjini Hamburger SV, Ujerumani.
Ronaldo Lima na Zenedine Zidane ni mabalozi wa taasisi ya Umoja wa Mataifa ya UNDP na walishirikiana na mastaa kibao wa sasa kama Didier Drogba wa Chelsea, Michel Salgado wa Blackburn, na mastaa wa zamani kama Luis Figo, Gheorghe Hagi, Pavel Nedved, Steve McManaman, Lucas Radebe, Fernando Hierro na wengineo kibao.
Mechi iliisha kwa marafiki wa Ronaldo na Zidane kushinda kwa magoli 5-4.
Pata utamu wa baadhi ya magoli katika video hii fupi. 



NDONDI: HAYE AJIPANGA KURUDI KWA KISHINDO

Aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu anaetambuliwa na WBC bondia David Haye (31) wa Uingereza amepania kuzichapa na kumtwanga KO bondia Vitali Klitschko (40) wa Ukraine ili kuwathibitishia mashabiki wake kuwa hajaisha.
Haye aliyepoteza mkanda wake wa WBC mwezi wa Julai baada ya kupigwa na mdogo wa Vitali aitwaye Vladimir, alistaafu ngumi lakini sasa amebadili uamuzi wake.
Vitali jana alithibitisha kuwa kwanza atapigana na Mwingereza mwingine aitwae Dereck Chisora Februari 18 mwakani mjini Munich kabla ya kumpa nafasi Haye.
Pambano la Haye vs Vitali linatarajiwa kufanyika kuanzia Julai. 2012 

TFF NAO WAMO SAKATA LA BASENA NA SIMBA
Kamati ya Ufundi ya TFF, nayo inahusika katika mgogoro wa Simba na Basena, TFF ilipaswa kukagua vyeti vya Basena mapema ili kuepuka migogoro.
Kamati ya Ufundi ya TFF sasa imeshituka na tayari kocha mpya wa Simba Milovan Cirkovic amewasilisha vyeti vyake.





BOXING:- FRANCIS CHEKA KUZIPIGA NA NYILAWILA
Francis Cheka

Bingwa wa ngumi za kulipwa Francis Cheka na mwenzie Karama Nyilawila, wanatarajiwa kupanda ulingoni Januari 28 mwakani.
Promota wa pambano hilo Philemon Kyando amesema pambano hilo litafanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Pambano ni la uzito wa Kg 72, litakuwa na raundi 10.


ZANZIBAR KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA VIVA
Timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) itashiriki katika michuano ya kombe la dunia kwa nchi zisizo mwanachama wa FIFA (NBF).
Mashindano hayo yatafanyika June mwakani nchini Iraq Kurdistan na kushirikisha nchi nane.

KIKAPU TAIFA


Matokeo ya Kombe la Taifa la Kikapu:-
Tabora iliichapa Kilimanjaro (102-58) Wanaume,
Mbeya vs Mara (62-50),
Singida vs Lindi (122-20),
Tanga vs Rukwa (114-19)

Mashindano hayo yanaendelea leo kuna mechi kati ya Shinyanga vs Singida (Wanaume) na Lindi vs Pemba (Wanawake).










KWELI CECAFA HAINA HURUMA NA WATANZANIA


Wakati Watanzania wanalia kwa uchungu kwa matokeo mabaya ya timu yao, CECAFA wao wanalilia mapato.
CECAFA imesema, imepata hasara katika michuano iliyofanyika nchini mwaka huu na kuongeza kuwa wameingiza jumla ya TSh Milioni 267 tu.
Ofisa habari wa TFF alisema hatua ya makundi imeingiza jumla ya TSh 145,613,000/=, Robo fainali TSh 58,470,000/=,Nusu fainali TSh 55,787,000/= na Fainali TSh 17,196,000/=.










TIMU YA TAIFA YA TENISI YAPATA KOCHA MTALIANO
Fabrizio Caldorone, kocha mpya wa timu ya taifa ya Tenis

Kocha wa kimataifa wa Tenisi kutoka Italia, Fabrizio Caldorone atainoa timu ya taifa ya Tenisi kwa kushirikiana na kocha mzawa Hassan Kassim.
Timu ya taifa ya Tenisi iko kambini kujiandaa na kombe la Taifa.

RIADHA

Chama cha Riadha nchini (RT), kimeamuru vyama vyake vyote vya mikoa kufanya chaguzi zao haraka ili wawakilishi katika uchaguzi wa taifa.
Bw. Suleiman Nyambui, Katibu Mkuu mkuu wa RT amesema mikoa ambayo bado ni Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Morogoro na Rukwa.

No comments:

Post a Comment

Post a Comment