MSALABA WA BOBAN, WA KUUBEBA NI JULIO
Boban Julio
Ikiwa ni siku chache tu toka kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) julio Kihwelo amtangaze Boban tena kwa madaha na majigambo, mchezaji huyo ameonyesha utovu wa nidhamu kwa kiwango cha kupitiliza.
Haruna Moshi (Boban) aliamua kuondoka katika benchi la wachezaji wa Kili Stars dakika 10 kabla ya mchezo kuisha kati ya Kili Stars na Zimbabwe. Kocha mkuu wa Kili Stars Mkwasa amesema, amefanya uamuzi wa kumfukuza Boban baada ya kumhoji kwa muda mrefu na hakukuwa na majibu. Boban ni mchezaji ambaye anaongoza kwa kuwa na nidhamu mbovu alishafukuzwa na kocha marcio Maximo, Jan Poulsen baada ya kukataa kujiunga na timu ya taifa.
NGORONGORO HEROES YAITA MOYO
Ngorongoro Heroes
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes, imetoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini. Ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 14 kwa kona safi iliyopigwa na Issa Rashid na kuingia wavuni moja kwa moja.
Baadae Afrika Kusini walisawazisha kwa Letsie Koapeng dk ya 21 kipindi cha kwanza. Hii inatia moyo hasa ukitazama mchezo uliopigwa ni wa kiufundi na msisimko wa hali ya juu.
DARTS
Alisema mashindano hayo yatafnyika katika ukumbi wa Urafiki na mpaka sasa timu 14 zimethibitisha kushiriki.
Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) leo inaingia dimbani kumenyana na kinara wa kundi A ambaye hajapoteza mchezo hata mmoja timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) katika robo fainali ya mashindano ya Kombe la CECAFA, na hivyo kufanya kibarua kuwa kigumu kwa Zanzibar.
Kabla ya kipute hicho cha Zanzibar Heroes, itatangulia mechi kati ya Burundi ikimenyana na Sudan.
No comments:
Post a Comment