Sunday, December 11, 2011

Dondoo

MOURINHO AENDELEZA UTEJA KWA GUARDIOLA
 
                   Mourinho                                      Guardiola

   Real Madrid imekubali kupewa kichapo na Barcelona katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 3-1 jana usiku.
Hii ni mechi ya 7 ya Clasico ambayo imeisha kwa ushindi wa Barcelona.
   Karim Benzema alifunga goli la mapema sana katika sekunde ya 23 lakini Alexis Sanchez alisawazisha kabla ya Xavi na Fabregas kupigilia misumari ya mwisho.
   Barcelona sasa inaongoza katika msimamo wa La Liga lakini iko mbele kwa mechi moja dhidi ya Real Madrid.









ANELKA HUYOOO MASHARIKI YA MBALI
Nicolas Anelka

Mshambuliaji hatari wa Chelsea Nicolas Anelka anatarajiwa kutangaza rasmi kusaini mkataba wa miaka miwili kuchezea timu Shanghai Shenhua ya China hapo dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari.
   Anelka anatarajiwa kutia kibindoni kiasi cha £175,000/= kwa wiki katika timu yake hiyo mpya. Kila la Kheri Bilal Nicolas Anelka.

VISA VYA MAN CITY TEVEZ VYAENDELEA
   Carlos Tevez

   Manchester City wamekubaliana na PSG ya Ufaransa juu ya uhamisho wa mchezaji Carlos Tevez kwenda kwa ada ya £21 Milioni.
   Lakini hilo linaashiria kuwashwa moto wa kutokuelewana baada ya Tevez mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kujiunga na AC Milan.
   Uhusiano mzuri uliopo kati ya tajiri wa Man City Sheikh Mansour wa Abu Dhabi na matajiri wa PSG wanaotokea Qatar ndiyouliofanikisha makubaliano haya.
   Tevez pia alikuwa anawindwa na Juventus, Inter za Italia na Corinthians ya Brazil.
   Tusubiri kuona ni wapi mchezaji huyo mkorofi atatua mwaka ujao.


No comments:

Post a Comment

Post a Comment