Thursday, December 29, 2011

Vituko vya Papic na Yanga

PAPIC NA YANGA VITUKO
Vichekesho vinavyoendelea baina ya Uongozi wa Yanga na kocha mkuu wa klabu hiyo Kostadin Papic ni vituko,  Papic ambaye anaifundisha Yanga kwa mara ya piliameitia tena klabu hiyo katika mgogoro mkubwa huku ikiwa imebaki siku chache wakutane na Zamalek.
Papic amekuwa akilalamikia maslahi yake na wachezaji ambapo amesema wachezaji hawana mshahara, kwake umeme na maji hakuna n.k, lakini cha ajabu Papic amekuwa akitoa kauli hizo kwa waandishi badala ya kuzungumza na uongozi.
Kama uongozi wa Yanga utaendelea kumchekea kocha huyu ni wazi kabisa atawapeleka pabaya.

Monday, December 26, 2011

Cheka na Mkanda wa Dunia

CHEKA: NATAKA MKANDA WA DUNIA
Bondia Francis Cheka "SMG" wa Morogoro, amesema hana wasiwasi wowote juu ya pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika Januari 28, 2012, kwenye uwanja wa Jamhuri dhidi ya Karama Nyirawila.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Morogoro jana, Cheka amesema kuwa amefanya maandalizi ya kushinda kwa kishindo ingawa dhamira yake sio pambano hilo bali Mikanda ya Dunia. 

Riadha na Kashfa Nzito

RIADHA ARUSHA YAKUMBWA NA KASHFA NZITO
Chama cha Riadha mkoa wa Arusha (ARAA), kimeingia katika kashfa nzito baada ya Mwenyekiti wake, Henry Nyiti kudaiwa kuibadili katiba ya chama hicho hali ambayo imezua mgogoro mzito ndani ya chama hicho.
Viongozi wa chama hicho wamemtuhumu Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa amepitisha katiba batili kwa manufaa yake binafsi, bila ya kujali kuwa na wao pia wanamchango mkubwa katika katiba hiyo.

Mchaki na Villa Squad

MCHAKI ABWAGIWA ZIGO KUINUSURU VILLA SQUAD
Frank Mchaki

Klabu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara Villa Squad ya jijini Dar es Salaam, imemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha soka wilaya ya Kinondoni (KIFA) Frank Mchaki kuwa Kaimu Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu wao, Iddi Godigodi kuwa mgonjwa.

Mafuriko Yawaathiri Nyota wa Soka

MAFURIKO YAWAATHIRI NYOTA WA SOKA
Mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo, zimewaathiri pia nyota wa zamani wa Simba na Yanga.
Nyota hao ni pamoja na kipa wa zamani wa Taifa Stars na Yanga Manyika Peter, Dua Said Nyota wa zamani wa Simba.
Spoti Kizaazaa inawapa pole wachezaji hawa pamoja na waathirika wote.

Simab na Yanga Kusaidiwa na DRFA

DRFA KUZISAIDIA SIMBA NA YANGA
Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), imepanga kuzisaidia timu za Simba na Yanga zinazojiandaa na michuano ya kimataifa.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, itacheza na Zamalek ya Misri katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Simba itacheza na Kiyovu ya Rwanda katika kombe la Shirikisho. 

Sunday, December 25, 2011

Yanga vs Power Dynamo

YANGA KUKIPIGA NA POWER DYNAMO

Timu ya Yanga itacheza na timu toka Zambia ya Power Dynamo siku ya mwaka mpya.
Yanga ambayo itacheza na ESCOM ya Malawi jumatatu katika mechi ya hisani, pia itacheza na Power Dynamo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi raundi ya pili, pia mechi yake dhidi ya Zamalek ya Misri.

Stars Kukipiga na Misri

STARS KUKIPIGA NA MISRI

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars), itakipiga na Mapharaoh wa Misri katika mechi ya kirafiki itakayopigwa kati ya Februari 23 au 24 jijini Cairo Misri.

Vituko Yanga vs Zamalek

VITUKO VYA YANGA NA MECHI DHIDI YA ZAMALEK

Wakati Yanga wakitumia vyombo vya habari kujinadi na kujigamba kwamba wataifunga Zamalek ya Misri, wenzao Zamalek watacheza mechi ya majaribio na Juventus ya Italia.
Zamalek itacheza na Juventus ya Italia kabla ya kuivaa Yanga ya jijini DSM, mpaka sasa Yanga inacheza mechi za majaribio na JKT Ruvu na Azam FC ya Mbagala.

BFT na OLIMPIKI

BFT YAANDAA MCHUJO KWA AJILI YA OLIMPIKI

Shirikisho la ngumi za ridhaa (BFT) linaandaa mchujo wa mabondia ili kupata mabondia Ishirini (20) watakaoweza kushiriki michuano ya Olimpiki 2012, itakayofanyika London, Uingereza.

Basena na Haki yake

BASENA AENDELEA KUDAI HAKI YAKE SIMBA
Moses Basena
Aliyekuwa kocha Mkuu wa Simba Moses Basena ameamua kuwasilisha malalamiko yake katika kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji.

Mada Maugo vs Joseph Kaseba

MADA MAUGO AJITAMBA KUMTWANGA JOSEPH KASEBA
 
Mada Maugo                        Joseph Kaseba
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Mada Maugo, amejitamba kumtwanga bondia Joseph Kaseba kwa (TKO) tarehe 28 Januari mwakani. 

Saturday, December 24, 2011

Floyd Mayweather 'JR' Atupwa Jela

FLOYD MAYWEATHER 'JR' ATUPWA JELA
Floyd Mayweather Jr akilia baada ya kupewa kifungo hicho

Bondia mashuhuri Floyd Mayweather Jr ametupwa Jela kwa siku 90, baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mpenzi wake wa zamani Jose Harris.
Pia amepigwa faini ya $2,500 na kutumia saa 100 kufanya kazi za kuhudumia jamii.

Mafuriko Yaharibu Kambi Twiga Stars

MAFURIKO YAHARIBU KAMBI TWIGA STARS
Mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam, yameharibu mazoezi ya timu ya Twiga Stars.
Timu ya Twiga Stars ambayob ipo kambini kujiandaa kucheza na Namibia imeshindwa kuendelea na mazoezi kutokana na wachezaji wake wengi kuathiriwa na mafuriko.

Mechi ya Simba na Gor Mahia

MECHI YA SIMBA NA GOR MAHIA YAOTA MBAWA
Ile Mechi iliyopangwa kuchezwa kati ya Simba vs Gor Mahia ya Kenya imeota mbawa, mechi hiyo imeota mbawa kutokana na timu ya Simba kutaka kitita cha Tsh milioni 25, wakati waandaji wa pambano hilo walitaka kuipata 20%.  

Simba, Yanga vs ESCOM

SIMBA, YANGA vs ESCOM (MALAWI) 
KUCHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO DAR
Timu za Simba na Yanga zitacheza na timu ya ESCOM kutoka Malawi, siku ya jumatatu na jumanne kwa ajili ya kuchangiawatu waliokumbwa na mafuriko.

Monday, December 19, 2011

GOLI TAMU LA KUJIFUNGA KUWAHI KUTOKEA!!!!!

Magoli ya kujifunga hayatokuwa "special" zaidi ya hili!!!
Mchezaji Mnigeria anaechezea timu ya Sun Hei SC ya Hong Kong alijifunga goli tamu kuwahi kuonekana duniani katika mechi dhidi ya timu ya Citizen AA.
Jionee mwenyeweeeeeeeee!!!!!!!!!!

Friday, December 16, 2011

Dondoo

SOKA: RATIBA YA MTOANO LIGI YA MABINGWA UEFA HADHARANI
Ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabinwga wa Ulaya (UEFA) raundi ya mtoano imetolewa. Timu 16 zilizobaki zimepangwa kukutana raundi ya kwanza tarehe 14/15 na 21/22 Februari na marudiano yanatarajiwa kufanyika tarehe 6/7 na 13/14 Machi. 
RATIBA:
Lyon (Ufaransa) vs APOEL (Cyprus)
Napoli (Italia) vs Chelsea (Uingereza)
Ac Milan (Italia) vs Arsenal (Uingereza)
Basel (Uswisi) vs Bayern Munich (Ujerumani)
Bayer Leverkusen (Ujerumani) vs Barcelona (Uhispania)
CSKA Moscow (Urusi) vs Real Madrid (Uhispania)
Zenit St. Petersburg (Urusi) vs Benfika (Ureno)
Marseille (Ufaransa) vs Inter Milan (Italia)

Thursday, December 15, 2011

Dondoo

PATA HABARI ZA MAKINI ZA MICHEZO YA NDANI, KIMATAIFA, UCHAMBUZI WA KINA...

SOKA: UNAFUNGA GOLI HALAFU RED CARD HIYOOOO!
Mshambuliaji wa Figuirense U20 ajulikanae kama Pottker ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga goli na goli hilo kumsababishia apewe kadi nyekundu.
Kosa lake ni kuwa aligombea mpira uliodundwa na refa na kufunga.
Kwa kawaida refa akidunda mpira wachezaji hufanya "fair play" kwa kutoa pasi kwa timu iliyokuwa inaumiliki kabla ya refa kupiga filimbi
Refa alikubali goli lakini akatoa red kadi kwa mfungaji.
Figuirense U20 ilishinda 4-1 dhidi ya Bahia U20
Jionee mwenyeweee!

SOKA: JERRY SANTO APATA ZALI ALBANIA
JERRY SANTO
Kiungo Mkenya Jerry Santo amejiunga na timu ya KF Tirana ya Albania kwa mkataba wa miaka miwili na nusu. Santo aliyeikacha Simba ya Tanzania na kuelekea Vietnam alipojiunga na timu ya HAGL mapema mwaka huu ambapo aling'ara vilivyo na kufanya klabu mbali mbali kuvutiwa nae.
Kwa sasa Santo anakamilisha nyaraka zake za kusafiria ili kukwepa matatizo yaliyowakuta wachezaji wenzake mshambuliaji Moses Arita wa Thika United na beki James Situma aliyekuwa Sofapaka ambao walichelewa kujiunga na timu zao za Ulaya kutokana na matatizo ya viza.
Santo aliyewahi kuchezea pia Tusker ya Kenya, sasa atajiunga na kundi la Wakenya kibao wanaocheza Ulaya kama kapteni wa Harambee Stars Denis Oliech, McDonald Mariga na Victor Wanyama ambao wote wanacheza klabu za ligi kuu za Ulaya.
Mara ya mwisho Santo kuitwa Harambee Stars ilikuwa kabla ya mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Shelisheli, ambapo alitemwa na kocha Francis Kimanzi.

Wednesday, December 14, 2011

Dondoo

PATA HABARI ZA MAKINI ZA MICHEZO YA NDANI, KIMATAIFA, UCHAMBUZI WA KINA...

SOKA: KESI YA UBAGUZI WA RANGI INAYOMKABILI 
SUAREZ YAANZA KUUNGURUMA.
Kesi ya kutoa maneno ya kibaguzi inayomkabili mchezaji Luis Suarez wa Liverpool imeanza kusikilizwa na Chama cha Soka cha Uingereza (FA) chini ya usiri wa hali ya juu.
Inaaminika kesi hiyo itachukua siku mbili kusikilizwa huku Suarez na Patrice Evra wa Manchester United wakitarajiwa kutoa ushahidi wao.
Kama FA itamkuta na hatia Suarez, nyota huyu wa Liverpool atarajie adhabu ya  kifungo kirefu cha kuichezea timu yake

SOKA: MECHI DHIDI YA UMASIKINI YAFANA
Mechi ya hisani ya kupambana na umasikini iliyozikutanisha timu ya Marafiki wa Ronaldo na Zidane dhidi ya Wachezaji Nyota wa Humberg Fc (Allstars) imefanyika usiku wa Jumanne 13/12/2011 mjini Hamburger SV, Ujerumani.
Ronaldo Lima na Zenedine Zidane ni mabalozi wa taasisi ya Umoja wa Mataifa ya UNDP na walishirikiana na mastaa kibao wa sasa kama Didier Drogba wa Chelsea, Michel Salgado wa Blackburn, na mastaa wa zamani kama Luis Figo, Gheorghe Hagi, Pavel Nedved, Steve McManaman, Lucas Radebe, Fernando Hierro na wengineo kibao.
Mechi iliisha kwa marafiki wa Ronaldo na Zidane kushinda kwa magoli 5-4.
Pata utamu wa baadhi ya magoli katika video hii fupi. 



NDONDI: HAYE AJIPANGA KURUDI KWA KISHINDO

Aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu anaetambuliwa na WBC bondia David Haye (31) wa Uingereza amepania kuzichapa na kumtwanga KO bondia Vitali Klitschko (40) wa Ukraine ili kuwathibitishia mashabiki wake kuwa hajaisha.
Haye aliyepoteza mkanda wake wa WBC mwezi wa Julai baada ya kupigwa na mdogo wa Vitali aitwaye Vladimir, alistaafu ngumi lakini sasa amebadili uamuzi wake.
Vitali jana alithibitisha kuwa kwanza atapigana na Mwingereza mwingine aitwae Dereck Chisora Februari 18 mwakani mjini Munich kabla ya kumpa nafasi Haye.
Pambano la Haye vs Vitali linatarajiwa kufanyika kuanzia Julai. 2012 

TFF NAO WAMO SAKATA LA BASENA NA SIMBA
Kamati ya Ufundi ya TFF, nayo inahusika katika mgogoro wa Simba na Basena, TFF ilipaswa kukagua vyeti vya Basena mapema ili kuepuka migogoro.
Kamati ya Ufundi ya TFF sasa imeshituka na tayari kocha mpya wa Simba Milovan Cirkovic amewasilisha vyeti vyake.





BOXING:- FRANCIS CHEKA KUZIPIGA NA NYILAWILA
Francis Cheka

Bingwa wa ngumi za kulipwa Francis Cheka na mwenzie Karama Nyilawila, wanatarajiwa kupanda ulingoni Januari 28 mwakani.
Promota wa pambano hilo Philemon Kyando amesema pambano hilo litafanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Pambano ni la uzito wa Kg 72, litakuwa na raundi 10.


ZANZIBAR KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA VIVA
Timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) itashiriki katika michuano ya kombe la dunia kwa nchi zisizo mwanachama wa FIFA (NBF).
Mashindano hayo yatafanyika June mwakani nchini Iraq Kurdistan na kushirikisha nchi nane.

KIKAPU TAIFA


Matokeo ya Kombe la Taifa la Kikapu:-
Tabora iliichapa Kilimanjaro (102-58) Wanaume,
Mbeya vs Mara (62-50),
Singida vs Lindi (122-20),
Tanga vs Rukwa (114-19)

Mashindano hayo yanaendelea leo kuna mechi kati ya Shinyanga vs Singida (Wanaume) na Lindi vs Pemba (Wanawake).










KWELI CECAFA HAINA HURUMA NA WATANZANIA


Wakati Watanzania wanalia kwa uchungu kwa matokeo mabaya ya timu yao, CECAFA wao wanalilia mapato.
CECAFA imesema, imepata hasara katika michuano iliyofanyika nchini mwaka huu na kuongeza kuwa wameingiza jumla ya TSh Milioni 267 tu.
Ofisa habari wa TFF alisema hatua ya makundi imeingiza jumla ya TSh 145,613,000/=, Robo fainali TSh 58,470,000/=,Nusu fainali TSh 55,787,000/= na Fainali TSh 17,196,000/=.










TIMU YA TAIFA YA TENISI YAPATA KOCHA MTALIANO
Fabrizio Caldorone, kocha mpya wa timu ya taifa ya Tenis

Kocha wa kimataifa wa Tenisi kutoka Italia, Fabrizio Caldorone atainoa timu ya taifa ya Tenisi kwa kushirikiana na kocha mzawa Hassan Kassim.
Timu ya taifa ya Tenisi iko kambini kujiandaa na kombe la Taifa.

RIADHA

Chama cha Riadha nchini (RT), kimeamuru vyama vyake vyote vya mikoa kufanya chaguzi zao haraka ili wawakilishi katika uchaguzi wa taifa.
Bw. Suleiman Nyambui, Katibu Mkuu mkuu wa RT amesema mikoa ambayo bado ni Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Morogoro na Rukwa.

Tuesday, December 13, 2011

Dondoo

KOSA GOLI YA MWAKA

Ama kweli duniani kuna mambo, mshambuliaji Oscar Cardozo wa Benfica amejizolea sifa za kukosa goli bora la mwaka, hebu jionee hii video fupi uwe shahidi.










MICHUANO YA KIKAPU TAIFA YATIMUA VUMBI
Mashindano ya Kikapu yaliyoanza juzi, yanaendelea kwa kasi ambapo jana timu ya Shinyanga Wanaume iliifunga Pemba Wanaume vikapu 82-46.Pemba Wanawake ilifanya kweli kuifunga Kilimanjaro Wanawake kwa vikapu 118-7, Mbeya imeicharanga Mara 62-49 upande wa wanawake. Singida Wanaume Imeifunga Lindi Wanaume 122-20. Mechi za leo ni kati ya Tabora vs Kilimanjaro (Wanaume), Morogoro vs Unguja (Wanawake), Mbeya vs Pemba (Wanawake), Unguja vs Rukwa (Wanaume).

NDONDI

Mabondia Mtuchoma Costa na Yonas Godfrey watapanda ulingoni Desemba 25 kusherehekea sikukuu ya X-Mass katika ukumbi wa Friends Corner Manzese.

TENIS

Michuano ya Tenis ya Davis kanda ya Sita kwa wachezaji wenye umri wa miaka 14-25 itakayofanyika 2012 jijini Dar es Salaam. Tayari timu ya Dar es Salaam imeweka kambi Tanga kwa msaada wa Kampuni ya Tanga Cement.

CHAMIJATA
Chama cha Michezo ya Jadi nchini (CHAMIJATA) kimetembeza bakuli. Mwenyekiti wa CHAMIJATA mzee Kazi Ngumbe amesema wanatafuta mdhamini ili kufikia malengo ya 2012, pia kuandaa uchaguzi mkuu wa chama.

Monday, December 12, 2011

Dondoo

WACHINA WAMTAMBULISHA RASMI ANELKA
Anelka akiwa amepozi na jezi ya timu yake mpya.

Nicolas Anelka amekuwa majeruhi wa kwanza wa kocha Andre Villas Boas wa Chelsea baada ya kuihama timu hiyo na kujiunga na Shanghai Shenhua ya China.
Anelka amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kutia kibindoni Â£175,000/= kwa wiki.
Kila la heri Bilal Nicolas Anelka.

Sunday, December 11, 2011

Dondoo

MOURINHO AENDELEZA UTEJA KWA GUARDIOLA
 
                   Mourinho                                      Guardiola

   Real Madrid imekubali kupewa kichapo na Barcelona katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 3-1 jana usiku.
Hii ni mechi ya 7 ya Clasico ambayo imeisha kwa ushindi wa Barcelona.
   Karim Benzema alifunga goli la mapema sana katika sekunde ya 23 lakini Alexis Sanchez alisawazisha kabla ya Xavi na Fabregas kupigilia misumari ya mwisho.
   Barcelona sasa inaongoza katika msimamo wa La Liga lakini iko mbele kwa mechi moja dhidi ya Real Madrid.









ANELKA HUYOOO MASHARIKI YA MBALI
Nicolas Anelka

Mshambuliaji hatari wa Chelsea Nicolas Anelka anatarajiwa kutangaza rasmi kusaini mkataba wa miaka miwili kuchezea timu Shanghai Shenhua ya China hapo dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari.
   Anelka anatarajiwa kutia kibindoni kiasi cha £175,000/= kwa wiki katika timu yake hiyo mpya. Kila la Kheri Bilal Nicolas Anelka.

VISA VYA MAN CITY TEVEZ VYAENDELEA
   Carlos Tevez

   Manchester City wamekubaliana na PSG ya Ufaransa juu ya uhamisho wa mchezaji Carlos Tevez kwenda kwa ada ya £21 Milioni.
   Lakini hilo linaashiria kuwashwa moto wa kutokuelewana baada ya Tevez mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kujiunga na AC Milan.
   Uhusiano mzuri uliopo kati ya tajiri wa Man City Sheikh Mansour wa Abu Dhabi na matajiri wa PSG wanaotokea Qatar ndiyouliofanikisha makubaliano haya.
   Tevez pia alikuwa anawindwa na Juventus, Inter za Italia na Corinthians ya Brazil.
   Tusubiri kuona ni wapi mchezaji huyo mkorofi atatua mwaka ujao.


Saturday, December 10, 2011

Dondoo

ASANTE KOTOKO WAINGIA DAR
Asante Kotoko wakiwasili jiji Dar es Salaam

   Timu ya Asante Kotoko toka Ghana imeingia Dar es Salaam kupambana na timu ya Simba katika pambano la miaka 50 ya Uhuru, kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Wakati huo huo leo ktakuwa na pambano kali kati ya Kilimanjaro Stars na Sudan kuwania nafasi ya tatu kombe la CECAFA, ikifuatiwa na fainali ya aina yake kati ya Rwanda na Uganda.
   Mapambano yote yatafanyika katika uwanja wa Taifa leo kuanzia saa 8:00 mchana.


KOMBE LA MAPINDUZI NETIBOLI

   Timu za netiboli kutoka Zambia na Zimbabwe zimethibisha kushiriki Kombe la Mapinduzi, pia timu kutoka Kenya na Uganda zimeshatumiwa mwaliko.
   Rahma Bakari, Katibu Mkuu wa (CHANETA) alisema tayari timu hizo zimethibitisha kushiriki na mashindano yanatarajiwa kuanza Januari mwakani.
   Mashindano hayo yanatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi milioni 100.


TUHUMA ZA MAKOCHA CECAFA ZATUPILIWA MBALI

   Tuhuma zilizopelekwa CECAFA na makocha mbalimbali wa timu shiriki zimetupiliwa mbali na uongozi, tuhuma hizo zimeelekezwa kwa marefa ya kwamba wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa baadhi ya timu.
   Akizungumzia tuhuma hizo, Katibu Mkuu wa CECAFA bw. Nicholas Musonye aemesema tuhuma hizo si za kweli na marefa wote walichezesha sawa kwa kuzingatia sheria za FIFA.  

Friday, December 9, 2011

Dondoo

RWANDA, UGANDA FAINAL STARS HOI


NAFASI YA 3
SUDAN  vs  TANZANIA                8:00 (Mchana)

FAINALI
RWANDA  vs  UGANDA               10:00 (Alasiri)


Timu Rwanda na jirani zetu Uganda wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali katika michuano ya CECAFA, Rwanda imefuzu kwa kuitoa Sudan mabao 2-1na Uganda wakiicharanga bila huruma wenyeji Kilimanjaro Stars kwa mabao 3-1 ndani ya muda wa ziada yaani (Extra Time).
Kilimnjaro Stars itakutana na Sudan kugombania nafasi ya tatu.


NYOTA WA NGORONGORO HEROES KUFANYIWA 
MAJARIBIO MAMELODI SUNDOWNS
Mshambuliaji wa Ngorongoro Heroes, Simon Msuvan huenda akaenda kufanya majaribio katika timu ya Mamelodi Sundowns kama watamwachia viongozi wake.


MBIO ZA MAGARI
Uhuru Rally Cross 2011 yanatarajiwa kwanza kutimua vumbi Jumapili katika eneo la Meserani nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mshindi wa kwanza atapata kitita cha shilingi milioni moja (1,000,000/=).

Thursday, December 8, 2011

Dondoo

SOKA: NUSU FAINALI CHALENJI HAPATOSHI!

      SUDAN  vs  RWANDA 
               
     UGANDA  vs  TANZANIA               

Leo ndio leo... Timu ya taifa ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" leo 10:00 alasiri inashuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Chalenji kwenye uwanja wa Taifa.
Kili Stars ambao ni mabingwa watetezi wameingia hatua hii baada ya kuifunga timu ya taifa ya Malawi "The Flames" kwa bao 1-0. Nayo timu ya taifa ya Uganda wao waliitoa timu ngumu ya taifa ya Zimbabwe kwa bao 1-0.
Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa saa 8:00 mchana utakaozikutanisha timu ya taifa ya Rwanda "Amavubi" dhidi ya timu ya taifa ya Sudan "Desert Hawks".
Washindi wa mechi za leo wanatarajiwa kuumana katika fainali siku ya Jumamosi 10.12.2011 katika uwanja wa Taifa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kili Stars.
  
SOKA: WANAWAKE WAPATA MWENYEKITI
Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) mkoa wa Pwani kimepata Mwenyekiti mpya na wajumbe katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi hizo, baada ya nafasi hizo kuwa wazi kwa kipindi kirefu.
Katika uchaguzi huo ulio uliofanyika katika ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), ambapo Isege Mabula alichaguliwa kuwa Mwenyekiti. Nafasi ya Katibu Msaidizi ilinyakuliwa na Saumu aliyekuwa mgombea pekee. Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu ilienda kwa Lydia Masena aliyemshinda Magdalena Mwinuka.
Wajumbe 9 kutoka wilaya za Mafia, Rufiji na Mkuranga hawakuhudhuria uchaguzi huo.

Wednesday, December 7, 2011

Dondoo

NURDIN AIPELEKA STARS NUSU FAINALI
Nurdin Bakari akishangilia goli

   Bao pekee lililofungwa na kiungo mahiri wa Kilimanjaro Stars na Yanga Nurdin Bakari, limeiwezesha Kili Stars kuingia hatua ya nusu fainali.
   Nurdin alipiga shuti kali kutoka kutokana na pasi safi iliyotoka kwa Mrisho Ngassa.
   Kwa matokeo hayo Kili Stars imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na itakutana na Uganda (The Cranes).


TFF, VYOO UWANJA WA TAIFA AIBU TUPU

   Licha ya kuwa uwanja ni mzuri na bora Afrika Mashariki na kati bado kuna tatizo kubwa na la kutia aibu.
   Vyoo vya uwanja wa taifa ni vichafu kiasi ambacho inahatarisha afya ya watumiaji na mifumo yote imeziba na hakuna wahudumu wa kusafisha.
   Hii ni hatari kwa afya na aibu hasa katika kipindi hiki cha mashindano ya Kombe la CECAFA.


NGORONGORO HEROES YAFA KISHUJAA
Pamoja na kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali, Ngorongoro Heroes imefanya maajabu kwa kuichabanga Mauritius 3-0, magoli ya Ngorongoro yalipitia kwa dakika 41 na Simon Msuvan Happygod, dakika ya 76 beki wa Mauritius alijifunga mwenyewe na dakika 85 Happygod alipachika wavuni goli la 3 kwa shuti kali.
Ngorongoro Heroes ilishindwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kuwa na pointi tano huku kinara wa kundi hilo akiwa na pointi saba.    

Tuesday, December 6, 2011

Dondoo

PAMBANO LA ASANTE KOTOKO NA SIMBA
 VS  

  Katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, Kampuni ya Future Century Ltd, wakishirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, inakuletea pambano la historia hapa nchini kwa kuwakutanisha wakongwe wa soka barani Afrika hao sio wengine ni Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) na Asante Kotoko ya Ghana, haijawahi kutokea.
  Mtanange huu utafanyika tarehe 11-Desemba, 2011 katika uwanja wa Taifa na sio shamba la bibi saa kumi jioni.
  Viingilio ni poa kabisa yaani TSh 30,000/= VIP A, 20,000/= VIP B, na 10,000/ VIP C wakati viti vya rangi ya Chungwa vitakuwa ni TSh 7,000/=, viti vya Blue vitakuwa TSh 5,000/= na kama haitoshi patakuwa na tiketi za TSh 3,000/= tu kwa viti vya Kijani.
  Wahi tiketi yako mapema katika vituo vyote vya Big Bon, Oil Com, Zizou Fashion na Steers, hali kadhalika utapata tiketi zako toka Clouds FM, Vanne Fashions Tabata, VETA Chang'ombe, Mwembe Yanga, shule ya Benjamini Mkapa, Uwanja wa Taifa na Robby Fashion Kinondoni.
  Pambano hili la kihistoria barani Afrika linaletwa kwenu na Future Century Ltd na PPF.
  Usiwe muoga wa matukio makubwa. Njoo uwe mmoja wa marafiki wa Uhuru na kutengeneza historia kubwa ya soka ambayo haijawahi kutokea barani Afrika.